USIHOFU
Hofu juu ya mambo yaliyopita; kwa kiasi kikubwa tumekuwa tukitawaliwa na hofu inayosababishwa na matendo yetu au jamaa zetu hata viongozi wetu matendo au maamuzi ambayo yalifanyika katika kipindi kilichopita,iwe katika fani tulizochagua,mchumba tuliyefunga naye ndoa,makosa tuliyowatendea ndugu zetu,ahadi tulizozivunja,maumivu tuliyowasababishia jamaa zetu,nafasi tulizoshindwa kuzitumia vizuri,kiwango cha chini tulichokionyesha,maneno tuliyosema au hata mazingira ya umasikini tuliyokulia...vyovyote vile,mambo haya yamekwisha tokea kabla na hakuna chochote tunaweza tukafanya kubadili matokeo yake lakini sisi bado tunaruhusu yatutie hofu.
Hofu juu ya mambo yatendekayo sasa; Lakini pia,utagundua kuwa watu wengi tuna hofu juu ya vitu au matukio fulani yanayotokea au kuendelea kutendeka,akili zetu zimejaa maswali Je, tunafanya maamuzi sahihi,tunafanya matendo sahihi,kwa mtindo na namna sahihi,katika wakati sahihi? Je,nini matokeo ya maneno tunayoyaongea,maamuzi tunayoyaamua,matendo tunayoyafanya,makubaliano tunayoafikiana au mpango tunaouanzisha,safari tunayokwenda? kwa kuwa hatuna uwezo wa kuamua matokeo ya vitu,mambo au matendo yetu tunayotenda hivi sasa,hali hii inatufanya tuwe na hofu.
Hofu juu ya mambo yajayo;Mungu ametuumba wanadamu kwa mfano wake,akatupatia akili ili tuweze kutambua mema na mabaya na akatupa uwezo wa kutawala viumbe wengine wote katika dunia hii,Lakini pamoja mambo haya yote ya msingi ambayo mungu ametujaalia hakuna binadamu yeyote ajuaye mambo yajayo hata sekunde moja tu ni mungu pekee mwenye mipango iliyokamilika ndiye aijuae mwanzo sasa na hata milele.....Tazama tunahofia afya zetu,familia zetu hapo baadae,tutakula tutakunywa na kuvaa nini,kipato chetu,ajira zetu na mafanikio yetu...hofu kubwa ni kitu fulani kisitokee au kitu fulani kitimie hapo baadae.
Kimsingi,karibu kila mtu kwa fulani amekuwa akihofu juu ya jambo fulani,pengine unaposoma makala hii mpendwa wangu kuna mambo yanakufanya uwe mwenye hofu kubwa ni lazima tukubali ukweli kwamba katika maisha haya tunayoishi hapa duniani ni lazima hofu itatukumba cha msingi ni kujua namna ya kukabiliana na hofu pindi inapotukabili.
Hofu inagawa akili zetu; utakubaliana na mimi kwamba tunapokuwa na hisia hii haribifu ya hofu akili zetu pamoja na utendaji wake kwa ujumla huathirika sana.
Hofu hunyonya nguvu zetu; hapa nazungumzia nguvu za kimwili,iwe ni katika michezo,kazini hata nyumbani tunaporuhusu hofu kuingia katika hisia zetu,inanyonya nguvu zetu hivyo.
Hofu hupunguza ufanisi na uzalishaji; tunashindwa kutumia uwezo na vipaji vyetu vizuri tuwapo michezono,viwandani,kazini,shambani a nyumbani pia kwa sababu ya hofu.
Hofu inaathiri afya zetu; matatizo ya kiafya na magonjwa kama vile kisukari,vidonda vya tumbo,shinikizo la damu na mengine mengi husababishwa kwa kiasi kikubwa na hofu ndani yetu.
Hofu huathiri maamuzi yetu; tunajikuta tukichelewa kufanya maamuzi ambayo pengine yalipaswa yafanyike haraka,au tunawahi kufanya maamuzi ambayo yalipaswa yafanyike baadae na kinyume chake,yote hii ni kwa sababu ya hofu.
Hofu inakwamisha maendeleo yetu; tazama sababu zote hizo kama vile hofu inapoiba amani na furaha nadani ya mioyo yetu,inagawa akili zetu,inanyonya nguvu zetu,inaathiri afya zetu na maamuzi kwa ujumla utagundua kwamba maendeleo yetu binafsi na jamii kwa ujumla yanakwama.
HOFU
Hofu ni hisia ambazo hutujaza wasiwasi na kutupa mshituka ndani yetu,hofu si dhambi ila namna tunavyokabiliana nayo hugeuka kuwa dhambi au kielelezo cha imani yetu na kukua kiroho,kama zilivyo hisia zingine za binadamu tupende tusipende lazima tutakuwa na hofu katika maisha tunayoishi katika dunia hii.
HOFU HUTOKA WAPI
Kitu cha uhakika ni kwamba mungu hajatuumba wanadamu ili tuishi
maisha yaliyojaa hofu na wasiwasi kwani alijua wazi kuwa hatuwezi
tukaishi maisha aliyokusudia kwetu, maisha yenye amani na furaha wakati huohuo tukawa na hofu juu
ya mambo ya kupita ya hii dunia,nayaita mambo ya kupita ya hii dunia
kwani laiti tungejua namna ambavyo nguvu za mbinguni zinavyoshinda
nakukesha zikitulinda,kutubariki na kutuwezesha katika kutimiza mpango
wa mungu tusingekuwa hata na jambo moja la kututia hofu,hivyo mungu hajatupa roho ya woga,hofu na wasiwasi bali shetani hutumia kila mbinu kutufanya tuhofu lakini pia sisi wenyewe tunaruhusu hisia zetu kuwa katika hofu kwani tukijikinga nayo hofu haiwezi ikaleta madhara katika maisha yetu.
KWA NINI UNAHOFU?
Ni kweli mungu ametuumba ili tuishi maisha yanayompendeza na kumpa utukufu,maisha ya furaha,amani,upendo,ukarimu,subira na imani...........baadhi ya mambo yafuatayo huiba amani yetu na kutufanya wenye hofu na wasiwasi,mambo haya yaweza kuwa kijamii,kiuchumi hata kisiasa pia.Hofu juu ya mambo yatendekayo sasa; Lakini pia,utagundua kuwa watu wengi tuna hofu juu ya vitu au matukio fulani yanayotokea au kuendelea kutendeka,akili zetu zimejaa maswali Je, tunafanya maamuzi sahihi,tunafanya matendo sahihi,kwa mtindo na namna sahihi,katika wakati sahihi? Je,nini matokeo ya maneno tunayoyaongea,maamuzi tunayoyaamua,matendo tunayoyafanya,makubaliano tunayoafikiana au mpango tunaouanzisha,safari tunayokwenda? kwa kuwa hatuna uwezo wa kuamua matokeo ya vitu,mambo au matendo yetu tunayotenda hivi sasa,hali hii inatufanya tuwe na hofu.
Hofu juu ya mambo yajayo;Mungu ametuumba wanadamu kwa mfano wake,akatupatia akili ili tuweze kutambua mema na mabaya na akatupa uwezo wa kutawala viumbe wengine wote katika dunia hii,Lakini pamoja mambo haya yote ya msingi ambayo mungu ametujaalia hakuna binadamu yeyote ajuaye mambo yajayo hata sekunde moja tu ni mungu pekee mwenye mipango iliyokamilika ndiye aijuae mwanzo sasa na hata milele.....Tazama tunahofia afya zetu,familia zetu hapo baadae,tutakula tutakunywa na kuvaa nini,kipato chetu,ajira zetu na mafanikio yetu...hofu kubwa ni kitu fulani kisitokee au kitu fulani kitimie hapo baadae.
Kimsingi,karibu kila mtu kwa fulani amekuwa akihofu juu ya jambo fulani,pengine unaposoma makala hii mpendwa wangu kuna mambo yanakufanya uwe mwenye hofu kubwa ni lazima tukubali ukweli kwamba katika maisha haya tunayoishi hapa duniani ni lazima hofu itatukumba cha msingi ni kujua namna ya kukabiliana na hofu pindi inapotukabili.
MADHARA YA HOFU
Hofu huiba furaha na amani ndani ya mioyo yetu; kwani mtu hawezi kuwa na furaha na amani wakati huo huo akawa na hofu,ni vitu viwili visivyoendana.Hofu inagawa akili zetu; utakubaliana na mimi kwamba tunapokuwa na hisia hii haribifu ya hofu akili zetu pamoja na utendaji wake kwa ujumla huathirika sana.
Hofu hunyonya nguvu zetu; hapa nazungumzia nguvu za kimwili,iwe ni katika michezo,kazini hata nyumbani tunaporuhusu hofu kuingia katika hisia zetu,inanyonya nguvu zetu hivyo.
Hofu hupunguza ufanisi na uzalishaji; tunashindwa kutumia uwezo na vipaji vyetu vizuri tuwapo michezono,viwandani,kazini,shambani a nyumbani pia kwa sababu ya hofu.
Hofu inaathiri afya zetu; matatizo ya kiafya na magonjwa kama vile kisukari,vidonda vya tumbo,shinikizo la damu na mengine mengi husababishwa kwa kiasi kikubwa na hofu ndani yetu.
Hofu huathiri maamuzi yetu; tunajikuta tukichelewa kufanya maamuzi ambayo pengine yalipaswa yafanyike haraka,au tunawahi kufanya maamuzi ambayo yalipaswa yafanyike baadae na kinyume chake,yote hii ni kwa sababu ya hofu.
Hofu inakwamisha maendeleo yetu; tazama sababu zote hizo kama vile hofu inapoiba amani na furaha nadani ya mioyo yetu,inagawa akili zetu,inanyonya nguvu zetu,inaathiri afya zetu na maamuzi kwa ujumla utagundua kwamba maendeleo yetu binafsi na jamii kwa ujumla yanakwama.
HOFU HAITUFAI
Mpendwa,mungu anajua kila kitu juu ya kila kitu,kila mahali na kila wakati...hapo kabla alipokuumba wewe na mimi alijua kuwa tunahitaji amani,furaha,upendo,chakula,mavazi na malazi,mafanikio na maendeleo na alijua wazi kuwa kukosekana kwa kimoja kati ya vitu hivyo muhimu kutatusababishia hofu,hofu ambayo itatutesa,hivyo mungu akaamua kututoa hofu kuhusiana na hofu katika maandiko matakatifu,maandiko ambayo ndiyo suluhisho na ufumbuzi wa kila tatizo na shida chini ya jua....Ukisoma kitabu cha Mtakatifu Mathayo,sura ya sita mstari wa thelathini na moja hadi thelathini na nne,maandiko yanasema "MSIHOFU, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta, kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote, Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake. na hayo yote mtazidishiwa, Basi MSIHOFU JUU ya kesho; kwa kuwa kesho ITAJIHOFU yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake".....Haya ni maneno yake Bwana wetu Yesu kristu,mwokozi na mfalme wa maisha yetu akituambia na kutufundisha kuwa hofu haitufai kama watu tuliomkabidhi maisha na hatma zetu . "MAJARIBU" NI DARAJA
"MAJARIBU"
Majaribu ni wakati ambapo tunakuwa tunakabiliwa na upinzani katika maisha yetu,upinzani katika afya zetu,uchumi wetu,kazi zetu,elimu yetu,familia zetu,ndoa zetu, upinzani huu waweza kuwa mkubwa au kidogo kulingana na mazingira,majukumu,umri hata jinsia...katika maisha yetu ni lazima tujaribiwe tukubali tukatae kama si sasa,leo basi kesho tutajaribiwa iwe kimwili hata kiroho....ni muhimu kutambua kuwa tutajaribiwa mara kwa mara kwani twaweza kushinda jaribu moja nakuingia katika jaribu jingine.
"MAJARIBU" HUTOKA WAPI?
Maandiko yanasema mungu kamwe hajakujaribu bali wewe mwenyewe kwa tamaa katika mawazo yako umejiweka majaribuni,maana yake ni kwamba mungu hajasababisha tuingie majaribuni bali tumesababisha sisi wenyewe.hisia katika akili zetu na machaguo katika maamuzi yetu yaendayo kinyume na amri za mungu ndiyo chanzo kikuu cha majaribu katika maisha yetu.
MATUNDA YA "MAJARIBU"
Utafurahi katika bwana
Imekua jambo la kawaida kulalamika,kuelekeza lawama kwa watu au vitu ambavyo kwa namna moja au nyingine tunahisi vimesababisha tujaribiwe,hii haitufai kama watu tunaomwamini yesu kristu,maandiko yanatuelekeza "Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini!" katika mateso,njaa,magonjwa,kutengwa hata kukataliwa yatupasa tufurahi katika bwana.
Utategemea uaminifu wa mungu
Mara nyingi tunapokabiliwa na jaribu fulani,imekuwa utamaduni wetu kutegemea uwezo na fikra zetu binafsi,hii ni kinyume na maandiko kwani biblia inasema "Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni
mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na
majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo
salama"
Utauona uwezo wa mungu
Laiti kama tusingejaribiwa na kila kitu kikawa kama tupendavyo sisi wanadamu basi ni dhahiri kuwa watu wengi wasingetambua uwepo wa mungu na mkono wake usio na mipaka,hivyo basi jaribu letu ni kithibitisho juu ya namna ambavyo mungu atatuwezesha kama maandiko yasemavyo kuwa "Mungu wangu atawapeni ninyi kila kitu mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake mtukufu katika Kristo Yesu".
Utakua zaidi kiroho
Tupitapo katika mjaribu tusisahau kwamba mungu yu pamoja nasi gongo lake na fimbo yake bwana vya tufariji kama maandiko matakatifu yasemavyo Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana uwezo wangu hukamilishwa
zaidi katika udhaifu." Basi, ni radhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili
uwezo wake Kristo ukae juu yangu.Kwa hiyo nakubali kwa radhi udhaifu, madharau, taabu, udhalimu na
mateso, kwa ajili ya Kristo; maana ninapokuwa dhaifu, ndipo ninapokuwa
na nguvu.
Ujumbe wa mungu utasambaa zaidi
Kadri tuapojaribiwa tunakua ki imani na ni faraja na matumaini makubwa kwa waumini wenzetu wanaposhuhudia tukishinda majaribu katika maisha yetu,pia majaribu yanatuwezesha kupata uwezo wa kuwafariji wengine pindi wajaribiwapo na hata kama tukianguka bado kwetu ni faida kama biblia isemavyo "Shauku
yangu na tumaini langu ni kwamba sitaaibika kwa njia yo yote, bali
nitakuwa na ujasiri,ili kama ilivyo sasa,Kristo aendelee kutukuzwa
kutokana na maisha yangu, kama ni kuishi au hata kama ni kufa.Kwa maana kwangu mimi,kuishi ni Kristo na kufa ni faida".
Makusudi ya mungu yatatimia
Ni kawaida katika hali ya kibinadamu kuhofu juu ya uweza wa mungu kutimiza mpango wake katika maisha yetu,hasa pale ambapo majaribu yanakuwa yameghubika kila sehemu ya maisha yetu,lakini ukweli ni kwamba jaribu ni kipimo cha imani na kwamba ukilishinda mkono wa mungu utadhihirika kwani "tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote
wampendao, wale ambao wameitwa kufuatana na mapenzi yake. Mungu hufanya
hivyo kwa faida yao".
"MAJARIBU" SI TATIZO,NI DARAJA
Katika mtazamo wa
kiroho,tatizo ni mzigo ambao hutuelemea na kutufanya tuchoke,tukate
tamaa, kukosa furaha na amani katika maisha yetu,lakini kwa upande
mwingine daraja ni njia ambayo hutuinua, kutuwezesha kushinda upinzani
na kuweza kujenga mahusiano ya karibu kabisa ya kiroho na muumba
wetu....mpendwa katika kristu maandiko yanasema "nasi
tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote
wampendao, wale ambao wameitwa kufuatana na mapenzi yake. Mungu hufanya
hivyo kwa faida yao",hivyo kwetu sisi tumpendao mungu twajua atatenda
kazi pamoja nasi hata katika majaribu na kufanya mambo yote kuwa mema
kwetu.
MSAADA HUU HAPA
Je,ulisha tambua kuwa unahitaji msaada wa mungu katika mapito ya hii dunia......?kama jibu ni ndiyo,basi upo katika wakati sahihi kwani katika maisha yaliyojaa vikwazo na majaribu kama tunayoishi ni wazi kwamba tunahitaji msaada wa mungu....ni wazi kwamba binadamu wenzetu wanaweza kutusaidia katika kiwango fulani kwa mfano msaada wa ushauri,pesa,chakula,mavazi,katika elimu au hata katika magonjwa,lakini hali ipo wazi kwamba binadamu wenzetu hawataweza kutupa msaada katika kila jambo,kila mahali na kila wakati bali mungu pekee ndiyo mwenye uweza huo.
- FARAJA TOKA KWA YESU
Usiku mmoja kabla ya yesu kristu kusulubiwa,aliutumia wakati wake vizuri kwa kuwaandaa wanafunzi wake juu ya mateso na vikwazo ambavyo vingefuata,aliwatia moyo kwa kuwaahidi ya kwamba "sitawaacha yatima,nitakuja kwenu nitamwomba mungu baba atawapatia msaidizi mwingine ambaye atakuwa nanyi milele" wakati kristu anawatia moyo wanafunzi wake kuhusu mateso na vikwazo vijavyo aliwaahidi kuwaletea msaidizi kama yeye na msaidizi huyo ni Roho Mtakatifu.
- ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU
Baada ya yesu kupaa mbinguni,kuume kwa mungu baba,mungu alisikia maombi yake na akatupatia msaada na zawadi ya roho mtakatifu ambaye huishi ndani yetu sisi ambao tumempokea yesu kristu kama mwokozi wetu,roho mtakatifu akishaingia ndani yetu hututambua kama wana wa mungu na kamwe hatatuacha milele,ni mmoja kati ya utatu mtakatifu yaani mungu baba,mwana na roho mtakatifu,ana nguvu,upendo,busara na yu kila mahali hivyo tunayo zawadi ndani yetu na yatupasa tujivunie wakati wote tunapopambana na shida,matatizo hata vikwazo.
- ROHO MTAKATIFU NI MSAADA
katika huzuni na mapungufu: Hutujaza nguvu pale tusipojiweza,yeye huwa kamilifu pale sis tunapokuwa na mapungufu na wakati tunapokuwa na hofu juu ya ahadi za mungu yeye hutukumbusha uaminifu wake kwa imani na nguvu zote zaidi ya vitu vingine vyote yeye hutufariji, wakati wa huzuni na majonzi kwani hugeuka furaha na tumaini letu.
Katika dhambi zetu:roho mtakatifu hutushitaki sisi wanadamu kuhusiana na dhambi zetu pia hutuhukumu mbele ya utukufu wa mungu,kupitia yeye ndiyo maana mimi na wewe tumetambua kuwa tunahitaji wokovu, vilevile hutufanya tutambue kwamba kristu pekee ndiyo njia kweli na uzima.
Katika neno la mungu:roho mtakatifu hutusaidia kusoma na kulielewa neno la mungu,sote twaelewa kuwa "mwanadamu wa kawaida hatambui mambo ya kiroho,ni kama upuuzi kwake na kamwe hawezi kuyaelewa kwani hutambuliwa kiroho" hivyo basi,roho wa mungu peekee ndiyo mtambuzi wa mambo hayo na hutufunza maana na namna ya kulitenda neno.
Katika sala na maombi:"kwa kuwa hatufahamu namna ya kuomba kama inavyotakiwa, roho mtakatifu hutunong'oneza kwa maneno ndani ya mioyo yetu" hii ina maana kwamba pale ambapo hatujui namna,wakati na kitu cha kuomba roho mtakatifu atatenda hivyo kwa niaba yetu.
Katika uwezo wa kiroho:roho mtakatifu hutupatia uwezo wa kiroho,hutujaza nguvu na uwezo wa kutenda yale yote ambayo mungu ametupangia,hutujaza uwezo wa utambuzi,ujuzi,nguvu na nia ya kuwawezesha watu wanaotuzunguka pia.
- TUIPOKEE ZAWADI HII
Je, twahitaji furaha,upendo,amani,ukarimu,subira,upole,uaminifu hata uwezo wa kujitawala......?sifa hizi zote ni matunda yake roho mtakatifu na hiyo ndiyo ahadi yake mungu katika maisha yetu endapo tutaipokea zawadi hii kwa kuanza na kumpokea na kumwamini yesu kristu kama mwokozi wetu.
- TAYARI YU NDANI YETU
Baadhi ya mambo yanaweza kutufanya tuhisi kama hatuna marafiki katika dunia hii,lakini hata tujisikie wapweke kiasi gani yatupasa kuamini kuwa hatupo peke yetu.Roho mtakatifu yu pamoja nasi na ndani yetu na ana mpango wa kuutimiza katika maisha yetu,nia yake kuu ni kuishi maisha ya kristu kupitia sisi na kwamba atatusaidia kukabiliana na kila changamoto katika mtazamo unaompendeza mungu.Anatumia mateso na huzuni kutufundisha upendo,busara na utukufu wa mungu vilevile anatuwezesha kuwa vile ambavyo mungu ametuumba na hakika atatupa ushindi katika kila jambo ambalo mungu ametupangia.
USIOGOPE
- Ukweli kuhusu woga.
Woga ni hisia gandamizi,woga husababisha hofu katika maisha yetu,woga hugawa akili zetu pia hudidimiza uwezo wetu wa kutenda mambo mbalimbali....Wasiwasi usiokuwa na maana unaweza kutukwamisha tusitimize mpango wa mungu katika maisha yetu,mungu alituumba wanadamu na akatuamuru tusiwe na hofu juu ya mambo yajayo.japokuwa wakati mwingine twaweza kuwa na wasiwasi lakini tusiruhsu hofu na woga kutawala maisha yetu.
- Kwa nini unaogopa?
kifo. pengine unaogopa kifo na hujui baada ya kifo nini mustakabari wako utakuwaje,nakushawishi umpokee yesu kristu kama mfalme na mwokozi wa maisha yako na kwa kufanya hivyo utakua umejihakikishia wokovu.
Majanga. pengine hofu na woga wako unatokana na uwezekano wa kutokea kwa matukio kama vile ajali za magari au moto,ukame,mafuriko,njaa au matetemeko ya ardhi ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kuhatarisha maisha yako.
Maadui. wapinzani wako,watesi wako ambao wameapa kukuangamiza pengine wanakutafuta kwa hali na mali..au maadui wanyama kama simba wakali ama wadudu kama nyoka na wengine wanafanya uwe mwenye woga na hofu.
Magonjwa. una kabiliwa na gonjwa sugu lisilokuwa na tiba au unahisi pengine hapo baadae utaandamwa na magonjwa hatarishi kama kisukari,kifua kikuu,kansa na magonjwa yasiyo na tiba kama vile ukimwi.
Kushindwa. unahofu na woga juu ya matokeo mabaya iwe ni katika biashara yako,elimu yako,shughuli zako mbalimbali kama kilimo au ufugaji au hata katika ajira yako au majaribio ya ajira.
- Jinsi ya kushinda hisia za uwoga.
Soma na tafakari neno la mungu. badala ya kusoma sehemu kubwa ya neno la mugu harakaharaka kila siku,nakushauri chagua maandiko mafupi inavyostahili soma uelewe kiundani na uyatafakari muulize mungu yana maana gani na namna ya kuyatekeleza katika maisha yako.
kumbuka uaminifu wa mungu katika maisha yako. kitu gani kilitokea hapo kabla ulipokuwa unakabiliwa na magumu? ulimlilia mungu ukatumia muda wako kusoma na kutafakari neno na ukaamua kuamini ahadi zake ulizozisoma katika neno lake na mungu akakujaalia nguvu na uwezo wa kushinda magumu hayo.
Tazama na ujifunze kutokana na ujasiri wa watu wengine.waumini ambao hupambana na magumu na changamoto za maisha huzishinda pale tu wanapotegemea uweza na nguvu za mungu,hivyo farijika na ukue katika imani pale ambapo watu wengine wanapotoa ushuhuda juu ya uaminifu wa mungu.
Jiulize,nisipomheshimu mungu itakuwaje? tambua kuwa kila tendo zuri au baya lina matokeo yake na kuwa siku zote tunavuna tulichopanda,hivyo kuukiuka mpango wa mungu yaweza kuwa rahisi mwanzoni lakini mwisho wake ni maumivu makali na kumwamini mungu siku zote huleta baraka.
Kumbuka ahadi yake ya kwamba atakuwa nasi siku na wakati wote . maandiko yanasema mimi na wewe tuna uhakika ya kwamba mungu muweza wa yote atatulinda na kutupa mafanikio katika maisha yetu.- Kumbuka ya nabii Yoshua.
Mungu alimwambia Yoshua kwamba "kuwa imara na mwenye nguvu usitishike wala usitetereke kwani bwana mungu wako ni pamoja nawe popote uendapo"(Yoshua 1;9)....Akiwa mfuasi wa Musa,Yoshua aliona namna ambavyo wana wa Israel walivyokuwa wakimpinga Musa,wakati mwingine walitaka hata kumponda mawe pale waliposhindwa kuelewana nae,hivyo baada ya Musa kufariki Yoshua alikuwa na jukumu la kuwaongoza wana wa Israel na kuwakabidhi nchi ya ahadi...ngumu kuliko vyote ilikuwa ni vita waliyopaswa kupigana dhidi ya wapinzani wao ili kuweza kumiliki nchi hiyo ambayo mungu aliwaahidi angewapatia.....Hivyo Mungu katika kutaka kumwondoa hofu Yoshua alimhakikishia uwepo na uweza wake akamwambia "kama nilivyokuwa na Musa,sitakuacha wala sitakuangusha,kuwa na nguvu na mwenye imani kwani utawaongoza na kuwakabidhi watu wangu nchi niliyowaahidi"(Yoshua 1;5-6)
- Ahadi ya mungu kwako.
Ahadi hizo ambazo mungu alimpa Yoshua wakati huo kwa kumwondoa hofu na woga juu ya changamoto ambazo zingemkabili katika kuwaongoza hadi kuwakabidhi wana wa Israel nchi yao ya ahadi hakika ni za kweli na halisi kwetu pia katika kupambana na changamoto na magumu yanayotukabili katika maisha yetu....Njia ya kushinda woga ni KUWA IMARA na WENYE IMANI...hapa Mungu anamaanisha kuwa imani ni zaidi ya kuwa na uhakika wa kufanikiwa katika magumu na changamoto zinazotukabili,ni hali ya KIAKILI na KIROHO itakayo tuwezesha KUKABILIANA na HATARI,VIKWAZO na CHANGAMOTO za MAISHA kwa UTULIVU,IMARA na BILA WOGA........Kwani kwa NGUVU na UWEZA wa MUNGU BABA tunatenda kwa imani.
USIKATE TAMAA
- Je, umekata tamaa?
pengine familia yako inateseka,umefukuzwa kazi,umepoteza mpendwa wako au labda taarifa za hivi karibuni
zinakufanya uhuzunike.Katika hali kama hii utajiuliza "mungu,hivi kweli upo? kwa nini hujatenda mpaka sasa?
- Je, kwa sababu gani umekata tamaa?
umeshindwa kuwaridhisha watu muhimu katika maisha yako? usipowaridhisha watu muhimu kama mke au mume,watoto,ndugu jamaa au mwajiri wako unaweza ukahisi kukata tamaa.
Hujapata jibu la maombi yako?
umemuomba mungu katika maeneo mbalimbali kama magonjwa,mchumba,ajira au
mafanikio lakini mungu hajajibu mpaka sasa,unahisi kukata tamaa.
Matatizo ya kiuchumi? unakosa pesa za kugharamia mahitaji muhimu kama chakula,mavazi na malazi, elimu na mahitaji mengine na unahisi kukata tamaa.
Matatizo ya kiafya?
unasumbuliwa na magojwa sugu,uzee au kutojiweza kwa muda mrefu
umemwomba mungu lakini hajajibu maombi yako mpaka sasa na umekata tamaa.
Upinzani?
katika ajira yako,katika familia yako,elimu yako au katika biashara na
sehemu zingine katika maisha yako umekua ukikumbana na upinzani na
vikwazo vinavyokufanya usisonge mbele na umekata tamaa.
Huthaminiki?
unahisi hupendwi na familia yako,jamii au hata mtu umpendae labda
unahisi hukubaliki katika jamii,familia au nchi fulani na hali hii imu ambao wao huhisi pengine kwa namna moja au nyingine wamechangia kuwa katika hali ya kukata tamaa.
Umeelemewa na mzigo wa dhambi? pombe,dawa zakulevya na anasa za hii dunia pamoja na dhambi zingine kama uzinzi,tamaa na usaliti vimekufanya ukate tamaa.
Hujapongezwa?
ni kweli umejituma katika kazi yako lakini mwajiri wako hajakupa
unachostahili,umefanya mengi kumridhisha mke au mume wako lakini
hathamini mchango wako kwake au umejitahidi kusoma kwa bidii lakini
hujafaulu katika masomo yako na umeka tamaa.
Dharau? unahisi familia yako,majirani zako,jamii au hata nchi nzima inakudharau na haikupi heshima unayostahili na umekata tamaa.
- Je, unayafahamu madhara ya kukata tamaa?
Kutokujiamini, watu waliokata tamaa hawajiamini katika mambo yao kwani huhisi pengine matokeo ya kila jambo lijalo yatafanana tu na jambo lililowafanya wakate tamaa.
Kukosa umakini, ukikatia tamaa upande mmoja katika maisha yako kwa mfano familia utajikuta kwamba unakosa umakini katika upande mwingine wa maisha yako mfano katika kazi yako.
Hasira na chuki, watu waliokata tamaa hujawa na hasira na chuki dhidi ya watu wengine,siyo tu wale wanaodhani wamepelekea kukata tamaa bali hata watu wasio husika.
Kujitenga, ukikata tamaa utajikuta unaanza kujitenga na watu wa karibu yako na jamii kwa ujumla na kuwasukuma mbali watu wanaowahitaji kama watoto, wake au waume zao kwa kisingizio kuwa maisha yamewaelemea
Maamuzi mabaya, mtu yeyote anaweza kufanya maamuzi yasiyo sahihi lakini watu waliokata tamaa wanahusishwa na idadi kubwa ya maamuzi mabaya kwani hufungwa na mtazamo hasi.
Kufilisika kiroho, kwa kuwa kuna sababu zilizo wafanya wakate tamaa mfano matatizo ya kiuchumi,magonjwa,upinzani,dhambi na mengine mengi hivyo hali hii hufungua mlango wa kutoamini uweza na utukufu wa mungu. - Hebu mtazame mfalme Daudi
Wakati mfalme Daudi na wenzake wakiwa mbali na mji wao.maadui walivamia mji wao wakateketeza mali zote na kuwateka wake na watoto wao,hofu kubwa iliwajaa pale walipopata taarifa kwamba wavamizi hao walikuwa na mpango wa kumuangamiza mfalme wao yaani Daudi,hivyo wakati mfalme Daudi anaumia na maumivu na usaliti pamoja hasara kubwa iliyosababishwa na wavamizi hao alikuwa anakabiliwa na hofu ya kupoteza uhai wake.Lakini mfalme Daudi "alijipa moyo katika bwana mungu wake"(1 sam 30;6) kwa maana nyingine Daudi hakukata tamaa bali alimgeukia mungu ambaye alimuahidi ushindi endapo atawakabili maadui hao(1 sam 30;18)
- Je, wajua?
Sasa jaribu kuhusisha vikwazo alivyopambana navyo mfalme Daudi na hivi ambavyo unapambana navyo wewe katika wakati kama huu......Tambua ya kwamba vikwazo,shida na matatizo mbalimbali humtokea mtu yeyote mahali popote katika dunia hii tunayoishi.....Pia vikwazo shida na matatizo haya yanayofanya tukate tamaa hujirudiarudia kwa maana kwamba unaweza ukavuka tatizo moja na punde ukapambana na tatizo jingine.....Vilevile matatizo na shida hizi hazitabiriki kwani hatujui wakati gani na mahali gani vitajitokeza......Mwisho,tukumbuke kwamba matatizo na shida hizi ni vya kupita tu na kwamba vitapita na kusahaulika endapo tutafanya maamuzi sahihi pindi vinapotukabili.
- Njia ya kuishinda roho ya kukata tamaa.
Badilisha mtazamo wako.....,kwanza naomba uanze kwa KUTAFAKARI kwa juu ya tatizo,shida na vikwazo vinavyokukatisha tamaa ukijua kwamba hata kama kwa hali ya kibinadamu haviwezekani jua kuwa kwa mungu hakuna linaloshindikana.....pili,GEUKA nyuma na utazame namna ambavyo mungu amekuwezesha kupita katika shida,matatizo na vikwazo ambavyo pengine ulidhani isingewezekana.......tatu,INUA KICHWA chako juu kwa kumwamini na kumtanguliza mungu katika kila jambo naye atakuonyesha njia ya kutokea katika hilo linalokusumbua na kukutesa.......mwisho TAZAMA mbele kwa matumaini juu ya mambo mengi mema ambayo mungu amekuandalia kwa ufupi "jicho halijawahi ona,sikio halijawahi sikia wala hayajawahi ingia katika moyo wa binadamu mambo ambayo mungu amewaandalia wale wampendao"
Fanya maamuzi sahihi sasa......anza kwa KUJIKABIDHI mikononi mwa mungu kwa kumpokea yesu kristu kama mwokozi na mfalme wako na kwamba alipokwenda msalabani alilipa dhambi zako zote.......pili TAMBUA kuwa mungu ana mpango na wewe katika maisha yako na kwamba atafanya mambo yote kuwa mema kwa wale tumpendao ambao tumeitwa katika mpango wake(warumi 8;28)......FAHAMU ya kwamba kuna furaha ya ajabu katika kumtegemea mungu(zab 103;19) na kwamba anakupenda na kamwe hatakutelekeza(Wahebrania 13;5).........na mwisho ZUIA fikra na mtazamo hasi unaokufanya ukate tamaa na utaona jinsi mtazamo chanya utakavyomruhusu mungu kugeuza matatizo na shida kuwa njia ya kujitukuza na kukupatia muujiza wako....BARIKIWA.