Akipita katika lango kuu la Yeriko kuelekea Yerusalem mahali ambapo alijua wazi kwamba atasalitiwa na kumwaga damu mikononi mwa wanadamu,Yesu akiwa ameongozana na wafuasi wake pamoja na watu wengi walioufuata msafara wake,hii ilikuwa safari yake ya mwisho kabisa kupita katika lango hilo na kwa takribani miaka mitatu alikuwa amekamilisha kazi ya kueneza injili na hivyo wakati ulikuwa umewadia wa mwokozi wetu kuinuliwa na kutukuzwa.
Yeriko ni lango la barabara inayoingia katika mji mkuu wa Yerusalem,hii ni barabara maarufu na kama hali ilivyo katika barabara zetu hii leo, watu wasiojiweza na wenye ulemavu hukaa pembezoni mwa barabara kuomba misaada kwa wapita njia ndiyo hali ilivyokuwa katika barabara ya Yeriko. Miongoni mwa wasiojiweza na walemavu hao alikuwapo kipofu ambaye kwa ulemavu wake huo, mkono wa mungu ulidhihirika na kuufanya umati ulioshuhudia muujiza huo kumtukuza mungu.
Upofu ulikuwa ugonjwa ulioambatana na ukoma na jamii ya wayahudi waliamini kuwa mtu mwenye ukoma ni mtu ambaye pengine kutokana na dhambi zake mwenyewe au wazazi wake alikuwa na laana ya mungu,hivyo vipofu na wakoma walitengwa,walinyanyaswa na kunyimwa haki zao za msingi.Miongoni mwao alikuwepo kipofu aliyekuwa amesikia habari zilizoenea kwa kasi kwamba Yesu kristu anatenda miujiza na kuponya magonjwa sugu pia kuwafungua waliofungwa na vifungo vya mwovu, kipofu huyu anajulikana kwa jina la Bathoromayo.
Kama inavyoaminika kwamba vipofu wana uwezo mkubwa sana wa usikivu na utambuzi wa sauti,mara baada ya kusikia kelele na vishindo vya umati wa watu walioambatana na Yesu, Bathoromayo alijua wazi kuwa wakati wa muujiza wake umewadia na akaanza kuita akisema.....
Bathromayo: "Yesu!,yesu!,yesu!,yesu!!!!!!!......"
Kutaka kutambua mtazamo wa umati ule juu ya watu wa tabaka la chini, Yesu pamoja na kumuona na kumsikia kipofu Bathromayo alimpita hata akaufanya umati ule udhani kuwa alikuwa mwenye haraka sana nao watu walithibitisha kuwa hawakutambua kazi na wajibu wa mwana wa mungu, wakamdhihaki na kumkatisha tamaa Bathromayo wakimwambia..
Umati: "Kimya wewe uliye laaniwa,hutambui kwamba yu mwenye haraka?"
Kwa kuwa hawakuwatambua na kuwathamini walemavu ,baada ya kusikika
akiita jina la yesu Bathromayo alinyamazishwa na kumriwa akae kimya mara
moja,lakini hakukata tamaa akaendelea kulia kwa sauti kubwa.....
Bathromayo: "Yesu!!!!!! mwana wa Daudi,nionee huruma!!!!"
Kuudhihirishia umati ule kwamba,mungu amemuinua kristu kuhubiri injili kwa wanyonge,waliotengwa na jamii,kuwaweka huru waliofungwa na vifungo vya mwovu na kutangaza wokovu kwa mataifa yote, mara akasimama na kumwita.....Bathromayo alitupa shuka lake pekee aliliokuwa akijisitiria kwa kipindi hicho chote cha upofu kwani alijua kuwa wakati wa muujiza wake ulikwisha wadia na kamwe hatalihitaji tena shuka lile.....alipofika,Yesu akamuuliza...
Yesu: "Nikutendee jambo gani.....?"
Bathromayo: "Nipate kuona !!!!!!!!!!!!!"
Yesu alimuuliza Bathromayo swali hili ili kupima imani aliyokuwa nayo juu yake ,jibu lake "nipate kuona tena" ni kielelezo kuwa imani aliyokuwa nayo juu ya kristu ilizidi hata imani ya wale waliokuwa wakimfuata na kushuhudia miujiza yote aliyokuwa akitenda kwani Bathromayo hakupata nafasi ya kujionea kwa macho bali kwa kusikia tu aliamini....Baada ya kusikia jibu lile na kutambua imani kubwa aliyokuwa nayo,Yesu kwa mikono yake miwili alimgusa macho yake na kumponya akisema.....
Yesu; Imani yako imekuponya,umesamehewa dhambi zako zote
Yesu; Imani yako imekuponya,umesamehewa dhambi zako zote
Mara baada ya mguso na neno moja tu la kristu,macho yaliyokuwa yamefumba kwa takribani miaka thelathini yalifumbuka,akapata kuiona tena taswira ya dunia na kumwona aliyemtendea miujiza sura yake yenye upako iking'ara kwa miale ya mbinguni,akanyanyua macho yake yaliyoponywa na kutazama juu mbinguni akaona mwezi na kumtukuza mungu kwa machozi na furaha akisema.
Bathromayo: "Nimeonaa!!!!! nimeona!!!!"
Yesu; Usimwambie mtu yeyote juu ya mambo haya, bali utimize mapenzi yake mungu baba aliye mbinguni."
Yesu; Usimwambie mtu yeyote juu ya mambo haya, bali utimize mapenzi yake mungu baba aliye mbinguni."
Umati: "Haaa,ni maajabu!!!!!,hata vipofu wanaponywa,hakika huyu ndiye masiya!!!!! miujiza!!!!!"
Yesu: "kwa nini hamuamini, lipi jambo gumu kwenu, au hamuamini ya kwamba mwana wa mungu anayo mamlaka ya kusamehe dhambi.....? Hakika nawaambieni yeyote mwenye imani aweza amuru mti huu ung'oke na ukatuame baharini na ikawa kama alivyonena, bali tu mkiomba ombeni kwa jina langu naye baba wa mbinguni atajibu maombi yenu kwani mimi ndiye njia, kweli na uzima na hakuna awezae kufika kwa baba pasipo kupitia kwangu."
Kisha Yesu, wafuasi wake pamoja na umati wa watu waliokuwa wakimfuata wakaendelea na safari yao kuelekea katika mji wa Yerusalem naye Bathromayo akaungana nao na kuwafuata huku akimsifu yesu na kumshukuru mungu kwa mambo aliyomtendea...
Ndugu yangu,mpendwa mkristu mwenzangu yawezekana wewe si kipofu lakini kama Bathromayo unalo tatizo, pengine unasumbuliwa na ugonjwa, umetengwa na jamii, umesalitiwa na uwapendao, umekataliwa, umasikini unakutatiza, ni mjane, ni yatima, umeathirika na madawa ya kulevya na pombe au umefungwa na vifungo vya mwovu, TAMBUA kwamba usomapo habari hii ni wito wako na Yesu anakuuliza "akutendee jambo gani?" Yawezekana kuna watu, vitu, hali au mazingira fulani yanakufanya ukate tamaa na usiweze kupata baraka zako toka kwa bwana kama ambavyo umati wa watu ulivyomkatisha tamaa Bathromayo, nakusihi jipe noyo THIBITISHA imani yako kwa kumkabidhi yeye mzigo uliokuelemea, naye kwa mguso au neno moja atakwenda KUKUPONYA, KUKUFARIJI, KUKUWEKA HURU, KUKUSAMEHE DHAMBI ZAKO ZOTE na KUKUPA UZIMA WA MILELE.