neno

"Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida na kusali daima" (Warumi 12;12)


"Mtu hafanywi kuwa mwadilifu mbele yake Mungu kwa kuisikia Sheria, bali kwa kuitii Sheria" (Warumi 2;13).


"Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU" (Mathayo 1;22-25).


"Fanyeni bidii ya kuongeza fadhila katika imani yenu: ongezeni elimu katika fadhila yenu, kuwa na kiasi katika elimu yenu, uvumilivu katika kuwa na kiasi, uchaji wa Mungu katika uvumilivu wenu, udugu katika uchaji wenu, na mapendo katika udugu wenu. Mkiwa na sifa hizo zote kwa wingi, zitawawezesheni kuwa watendaji na kupata faida katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo"
(2 petro 1;5)


"Mungu huwakubali watu kuwa waadilifu kwa njia ya imani yao kwa Yesu Kristo; Mungu hufanya hivyo kwa wote wanaoamini; hakuna ubaguzi wowote"
 (Warumi 3;22)

"Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao."
(1 Wakorintho 2;9)


"Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu,vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake" (2 Petro 3;10).


 "Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu"
 (Zaburi 118;8)

"Hatimaye ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo na sifa, yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote ya kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo uzuri wo wote, pakiwepo na cho chote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo" (wafilipi 4;8)


"Naona kuwa mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kamwe kama tukiyafananisha na ule utukufu utakaodhihirishwa kwetu"
 (Warumi 8:18)


"Upepo huvuma upendako,na sauti yake waisikia,lakini hujui unakotoka wala unakokwenda,kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho"
 (Yohana 3:8). 



"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema" (Mithali 28:13)


"Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa" (Mithali 29:23). 



"Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini, wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?"  (Mathayo 6:25)


"Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu" (Wagalatia 5:22)


"Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi"
 (Warumi 5:7) 



"Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aonyeshe
jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima."
 ( James 3:13)


"Kama watoto wa Mungu wenye utii, msikubali kamwe kufuata tena tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mlipokuwa wajinga.Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu. Maandiko yasema: "Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu." (1 Petro 14-16)


"Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao."
 (1 Wakorintho 2;9)


"Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?" 
(Wagalatia 3:1,3)


"Sasa, kwa vile tumekubaliwa kuwa wadilifu kwa imani, basi, tunayo amani na Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwa imani yetu, yeye ametuleta katika hali hii ya neema ya Mungu ambamo sasa tunaishi"  
(Warumi 5:1,2) 


"Si hayo tu, bali tunafurahi pia katika taabu tukijua kwamba taabu huleta saburi, nayo saburi huleta uthabiti, na uthabiti huleta tumaini.Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa, maana Mungu amekwisha miminia mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia" 
(Warumi 5:3,5)


"Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,  Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja" 
(Hesabu 16:20,21) 


"Wewe lengo lako ni kunidhuru, lakini Mungu alikusudia yote kwa ajili ya mema. Akanileta mpaka nafasi hii ili niweze kuokoa maisha ya watu wengi" 
(Mwanzo 20:50)

 
 "Na sasa hakuna hukumu kwa wale walio ndani ya kristu,wale watendao kiroho bali si kimwili" (Warumi 8:1)


"Ninawaambieni,yeyote atakaye kiri jina langu mbele ya watu nami nitamkiri mbele ya malaika wa mungu na yeyote atakayenikana mbele ya watu nami nitamkana mbele ya malaika wa mungu"  
(Luka 12:8,9)


"Kwani mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee,yeyote atakaye mwamini hataangamia bali atapata uzima wa milele"
 (Yohana 3:16)


"Bado hamjaamini ya kwamba mimi ni ndani ya mungu na mungu yu ndani yangu?na maneno niyasemayo siyatamki mimi mwenyewe bali baba yangu aliye ndani yangu huitenda kazi" (Yohana 14:110)
 
"Kwa neema umekombolewa kupitia imani,hukujikomboa mwenyewe bali ni zawadi toka kwa mungu,si kwa matendo yako ili usijisifu"
(Waefeso 2:8,9)


 "nipitapo katika bonde la mauti sitaogopa mabaya, bwana yu pamoja nami,gongo lake na fimbo yake bwana vyanifariji"
(Zaburi 23:4)

 
"Si kila aniitae bwana atauona ufalme wa mbingu,bali yule atendae mapenzi ya mungu aliye juu mbinguni" (Mathayo 7:21)

 
"Nitawabariki wote watakaokubariki,nitawalaani wote watakaokulaani na kupitia wewe mataifa yote ya ulimwengu yatabarikiwa" 
(Mwanzo 12:3)

 
"Heri masikini mwenye hekima kuliko yule mjinga anayepayuka kwa midomo yake" (Mithali 19:1)

 
"Niite nami nitakuitikia na kukuonyesha mambo makuu ambayo hujayafahamu" (Yeremia 33:3)


"Tazama,mkono wa mungu si mfupi hata ukashindwa kuokoa wala sikio lake si zito hata lisisikie"(Isaya 59:1)


" Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao" (Mathayo 7:11)


"Kila mwanamke mwenye akili huijenga nyumba yake,lakini mwanamke mpumbavu huivunja kw? a mikono yake mwenyewe" 
(Mithali 14:1) 


 "Sipo hai tena,nimesulubiwa pamoja na kristu si mimi ninayeishi bali kristu ndani yangu na maisha ninayoishi sasa katika mwili ninaishi kwa imani ya kristu  mwana wa mungu aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu" 
(Wagalatia 2:20)


 "Usiogope kwani nipo pamoja nawe,usitetereke kwani ndimi bwana mungu wako,nitakutia nguvu,nitakuinua kwa mkono wangu mtukufu wa kuume" 
(Isaya 41:10)

"Msiwe wasahaurifu kuwafurahisha wageni,kwani kwa kufanya hivyo wengi wamewafurahisha malaika bila kujua" 
(Wahebrania 13:2)


"Basi,imani ni kiwakilishi cha mambo yatumainiwayo,uthibitisho juu ya mambo yasiyoonekana"(Wahebrania 11:1)


"Furahini katika bwana,nawaambieni tena,furahini" 
(Waphilipi 4:4)



 "bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu"(Zaburi 23:1)


"Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka. Shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu ambayo ni ya thamani zaidi kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima Siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa"  
(1 Petro 1;6).
 
 "Msijali juu ya chochote bali kupitia  sala na maombi kwa shukrani mjuzeni  mungu maombi yenu"(Wafilipi 4;6)



 "Ninayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu"
(Wafilipi 4;13)


"Heri masikini wa roho maana ufalme wa mbingu ni wao"
(Mathayo 5;3)


"Heri wenye moyo safi maana watamwona mungu"
(Mathayo5;8)


 "Ninafahamu mpango nilio nao kwa ajili yenu,si kuwaangamiza bali ni kuwapa hazina ya mioyo yenu"(Yeremia 29:11)


 "Mtegemee mungu kwa mambo yako yote,mtangulize katika kila jambo na atakuonyesha njia"(Mithali 3;5)