mbegu
Ni mmea ambao hupandwa kwa madhumuni ya kuvuna zao kutokana na mmea huo,hii ndo maana halisi ya mbegu katika maisha ya kimwili lakini kiroho, mbegu yaweza kuwa kitendo, neno au kitu chochote unachokitoa, kusema au kutenda ambacho huzaa kitu, neno au kitendo.
Lengo
Kila kitu hufanyika kwa malengo maalum, hata mbegu hupandwa kwa malengo maalum kama vile kuweza kuvuna mazao hapo baadae, hii ndo hali halisi katika maisha ya kawaida, lakini katika maisha ya kiroho mbegu kwa maana ya tendo, neno au kitu chochote chema huzaa neno, tendo au kitu chema.
Zao
kama lengo letu lilivyo ni kupanda mbegu kwa nia ya kupata mazao, lakini mazao haya yatatokana na mbegu tuliyoipanda, kiasi au kiwango tulichopanda na wakati tuliopanda maandiko yanasema "tutavuna tulichokipanda, kadri ya mbegu zetu na baada ya kuzi siha ardhini.
mungu ametuagiza
Maandiko yana sema mungu ametuagiza kutoa sadaka si kwa sababu anahitaji msaada kutoka kwetu katika kutimiza na kufanikisha kazi yake, la hasha, katika agano la kale mungu anasema "Leteni sadaka zenu ghalani mwangu ili kuwe na chakula cha kutosha nyumbani mwangu, nijaribuni katika hili muone kama sitafungua madirisha ya baraka za mbinguni kwa ajili yenu hata msipate chumba cha kuzihifadhia" (malaki 3;10) pia bwana anatusihi tumrudishie asilimia kumi ya vipato vyetu na biblia inasema kuwa "yeyote asiyemrudishia mungu asilimia kumi ya kipato chake anatenda dhambi na kufunga baraka zake toka kwa muumba.
mtii mungu
tangu enzi za agano la kale mungu amekuwa akiwabariki watu wake ambao humtii na kufuata maagizo aliyoagiza yafuatwe, hata sisi leo tunaweza kupokea baraka zetu kutoka kwa mungu kwa kufuata na kutimiza maagizo yake ikiwa ni pamoja na kutoa sadaka. Hivyo mpendwa mkristu mwenzangu unaesoma ujumbe huu nakusihi umtii mungu katika hili.
Panda mbegu yako
pengine utajiuliza swali ni mahali gani upande mbegu yako leo,lakini naweza kukuhakikishia kwamba,kuna sehemu nyingi sisi kama wanadamu twatweza panda mbegu zetu leo,kumbuka mbegu si pesa pekee,twaweza nena mema kwa wanadamu wenzetu,wafariji wenye huzuni,kuwashauri na kuwatia moyo wenye mizigo mizito kiroho hata kimwili na kutenda matendo mema kila wakati,lakini pia...
- Sadaka kanisani.
- Toa msaada kwa watu masikini,walemavu na wenye mahitaji muhimu.
- Fanya maombezi kwa ajili ya dunia nzima na viumbe vyote.
- Wabariki watu wote wakati wote (tenda mema).
- Saidia taasisi zinazo hubiri injili na kutangaza wokovu wa Yesu kristu
Mwamini mungu sasa na nakuomba umtii kwa kupanda mbegu yako sasa na utastaajabu kwa namna ambavyo mungu atakulipa fadhila kwa kitendo chako kidogo cha ukarimu kwa kuwa na imani na kutii maagizo katika neno lake.