NANI AMEBARIKIWA?
Mtu mwenye mwonekano mzuri au sura nzuri,mali nyingi,cheo au afya njema ndiyo mtu aliyebarikiwa na Mungu?.....Ukweli ni kwamba kila mmoja wetu katika kristo amebarikiwa kwani baraka ni uwezo wa kiroho ambao tunaupata kutoka kwa Mungu ili kutuwezesha kusonga mbele katika maisha ya imani pamoja na shida, vikwazo, vishawishi, majaribu na mateso tunayokabiliana nayo. Katika kitabu cha mtakatifu Mathayo Yesu kristo anasema wamebarikiwa maskini wa roho, wenye moyo safi, wenye imani, wenye huzuni na wanaoteswa na kuonewa kwa ajili ya utakatifu.Ukweli ni kwamba hakuna binadamu yeyote anayeweza kuishi katika dunia hii bila kutegemea neema za mwenyezi Mungu, Hivyo mimi na wewe tunahitaji sana neema na baraka za Mungu.
KABLA MUNGU HAJAKUBARIKI.
Ni kweli kwamba ili tuvune mazao yatubidi tupande mbegu,ili mvua inyeshe mawingu sharti yatande,ili kiumbe kizaliwe mbegu mbili ya kike na kiume ziungane, hali hii ni asili katika maisha yetu.Ukweli ni kwamba kabla Mungu hajatubariki katika maisha yetu pia hutenda mambo ya msingi yafuatayo:
Hupima imani
Imani yako ni kithibitisho cha mambo yasiyo onekana, kigezo juu ya mambo yajayo na tusipokua na imani hatuwezi kumpendeza Mungu.Ukweli ni kwamba imani yetu ndiyo kipimo cha baraka zetu tutakazopokea, kumbuka Ibrahim kabla Mungu hajambariki kuwa baba wa mataifa yote alipima imani yake katika kiwango cha hali ya juu kabisa kwani ulipita muda mrefu sana kabla ahadi ya Mungu haijatimia, pia alimpima kwa kumwamuru amtoe sadaka mwanae wa pekee Isaka.
Huruhusu majaribu
Majaribu ni wakati ambao tunakua tunapambana na wakati mgumu pengine kiroho hata kimwili, kiasili majaribu tunaweza kuyaleta sisi wenyewe au Mungu huruhusu yatokee katika maisha yetu, majaribu hupima upendo na imani yetu kwa Mungu.Kumbuka Ayubu alijaribiwa katika kiwango cha juu kabisa kwani Mungu alimruhusu shetani aangamize watoto, mifugo na mali zake zote, kama haitoshi aliruhusu magonjwa kwa Ayubu.
Huruhusu mateso
kipigo,njaa,kiu, kumwaga damu, kifungo na usaliti,ilimradi tu roho itambue utukufu wa Mungu na kumlilia kumbuka katika bustani ya getsemane walimkamata, wakampeleka kwa Pilato, kwa Herode baadae kwa pilato tena akabeba msalaba hadi golighota, akasulubiwa na saa la tatu tetemeko la ardhi, radi na giza nene vilithibitisha 'imekwisha' akakata roho.... Huyu ni Yesu kristo mwana wa Mungu.
Hutoa wajibu
Wajibu ni kazi au majukumu ambayo yatupasa kuyatimiza katika maisha yetu kama wafuasi wa kristo ,imeandikwa asiyefanya kazi na asile,kumbuka Nuhu Mungu alimpa wajibu wa kujenga safina hatua mia tatu urefu, upana sabini na awaingize viumbe wawili wawili na mimea wa kila aina ndani ya safina, Mungu alimwagiza kujenga safina akasema ataamuru mvua kubwa na mafuriko katika taifa ambalo mvua haikuwahi kunyesha karne kadha zilizopita.
Huleta maadui
Adui anaweza kuwa binadamu, mnyama au kitu chochote ambacho hutokea mbele yako kikihatarisha uwepo wako, maendeleo yako au hata afya yako.Kumbuka Daudi alikua mchunga kondoo, chini ya miaka kumi na nane aliyeagizwa kupeleka chakula cha wapiganaji waliokuwa wakijianda lakini kwa hofu kumkabili aliyekuwa kiburi katika vita mfilisti Goliathi.Daudi kwa imani alikusanya mawe kadhaa na kombeo lake na akamkabili Goliathi.
Huleta upinzani
Iwe kiroho au kimwili mtu au kitu kinachotenda kinyume na wewe au shughuli au kazi yako, sote huelewa na kupenda upinzani katika michezo kwani huburudisha,lakini upinzani aliopambana nao Saulo ambaye baadae aliitwa Paulo hakika ni wa ajabu dharau kuchekwa,kupigwa mawe, kulala nje,kunyeshewa na mvua, njaa, kufungwa jela,mijeledi na upinzani hatari dhidi ya kueneza injili ya yesu.
Husubiri utayari
Uwezo, imani na utayari wako katika kupokea baraka na neema za Mungu ni muhimu sana kabla hujapokea baraka hizo kumbuka mungu ni mwaminifu na kamwe hawezi akaruhusu baraka zitakazotuathiri hivyo ni lazima tuonyeshe utayari wa kuzipokea, kumbuka kipofu aliyekaa katika milango ya Yeriko akiwa ombaomba tangu kuzaliwa kwake aliposikia kelele za msafara wa Yesu aliyekuwa amesikia habari juu ya yesu mponyaji na mwokozi alilia kwa sauti na kuita 'Yesu Yesu,mwana wa Daudi nionee huruma' mtu mmoja akajibu 'wacha utamchelewesha' kwani ile ilikua safari yake ya mwisho kuelekea yerusalem, mara Yesu akasimama na kumwita, aliruka na kumfuata kisha Yesu akamuuliza 'unataka nikufanyie nini?'naye akajibu 'nipate kuona' ...jina lake ni Bathlomeo
JIANDAE KUBARIKIWA LEO.
Mungu anakubariki leo, utapata nguvu na uwezo wa kushinda na kufanikiwa katika maisha yako.Mungu anajaribu IMANI yako kama Ibrahim alivyovumilia na kusubiri ahadi kwa muda mrefu, vumilia pia.....Mungu anaruhusu MAJARIBU katika maisha yako, kama Ayubu alivyovumilia baadae Mungu alimpa mara mbili ya alichopoteza,Vumilia pia utapata mara mbili zaidi ya ulichopoteza,...........Mungu ameruhusu MATESO kama yesu kristo aliteswa akasulubiwa, akafa na siku ya tatu akafufuka yupo mbiguni na atarudi kutuchukua mimi na wewe..... Mungu amekupa WAJIBU,kazi kama ya Nuhu,alifanya kama Mungu alivyoagiza bila kujali watu walio mkejeli kwa kujenga safina katika nchi ambayo mvua haikunyesha kwa miaka mingi kabla, lakini alijenga na Mungu alileta mvua na ikawaangamiza wote isipokua Nuhu na familia yake, Timiza wajibu wako ambao Mungu amekupa na utabarikiwa,............Mungu ameruhusu MADUI kama Daudi aliamini Mungu angempa ujasiri wa kumkabili Goliathi ambaye alikua anamzidi nguvu, urefu, umri hata siraha hivyo basi usiangalie ukubwa wala hatari kuhusiana na maadui,watu,wanyama hali au vitu vyovyote.. mtegemee Mungu na si uwezo wako, kama Daudi utashinda maadui.
Mungu ameruhusu UPINZANI katika maisha yako, elimu yako, biashara yako, afya yako hata katika kazi yako,.........Paulo aliamua kuendelea kueneza injili ya Yesu ndiyo sababu sehemu kubwa ya agano jipya aliandika yeye vitabu kama warumi, wagalatia, wahebrania, wafilipi na waefeso na vingine vingi ambavyo leo vinasababisha mimi na wewe tunabarikiwa, hivyo usijali upinzani songa mbele
Mungu anangojea UTAYARI wako wa kupokea na kulinda baraka zake kwako, kama Bathlomeo aliposikia msafara wa yesu alithibitisha utayari na imani yake... zaidi ya kuona, Yesu pia alimsamehe dhambi zake zote, nawe pia onyesha utayari wa kupokea baraka na neema za Mungu kwa kumlilia katika sala na maombi zaidi ya kubarikiwa utasamehewa dhambi zako zote.